Mtunzi: Hilali John Sabuhoro
> Mfahamu Zaidi Hilali John Sabuhoro
> Tazama Nyimbo nyingine za Hilali John Sabuhoro
Makundi Nyimbo: Zaburi | Kwaresma
Umepakiwa na: Halisi Ngalama
Umepakuliwa mara 1,469 | Umetazamwa mara 4,574
Download Nota Download MidiUturehemu Ee Bwana kwa kuwa tumetenda dhambi X2
1:Ee Mungu unirehemu sawasawa na fadhili zako kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu unioshe kabisa na uovu wangu.
2:Maana nimejua mimi makosa yangu na dhambi yangu I mbele yangu daima nimekutenda dhambi wewe peke yako na kufanya maovu mbele za macho yako.
3:Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho yangu iliyotulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho yako mtakatifu.
4:Unirudishie furaha ya wokovu wako unitegemeze kwa roho ya wepesi Ee Bwana uifumbue midomo yangu na kinywa changu kitazinena sifa zako.