Mtunzi: Alan Mvano
> Mfahamu Zaidi Alan Mvano
> Tazama Nyimbo nyingine za Alan Mvano
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Alan Mvano
Umepakuliwa mara 1,838 | Umetazamwa mara 5,825
Download NotaKiiitikio
( Karibu karibu Yesu wangu, karibu Bwana moyoni mwangu, karibu Bwana ukae nami siku zote ) x2
Mashairi
1. Wewe ndiwe uzima wangu pia mwanga kila niendako, nakukaribisha uwe nami siku zote
2. Nakuomba uniimarishe nisisumbuliwe kamwe na shetani, nakukaribisha uwe nami siku zote
3. Ninatambua fika kwamba bila nguvu zako siwezi kitu, nakukaribisha uwe nami siku zote
4. Nakuomba unijalie roho ya upendo kwa jirani zangu, nakukaribisha uwe nami siku zote