Mtunzi: Alan Mvano
> Mfahamu Zaidi Alan Mvano
> Tazama Nyimbo nyingine za Alan Mvano
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Alan Mvano
Umepakuliwa mara 2,557 | Umetazamwa mara 5,941
Download Nota Download MidiKiitikio
Mpeni Bwana , mpeni utukufu na nguvu, mpeni Bwana mpeni Bwana,
mpeni Bwana utukufu na nguvu
Mashairi
1. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, mwimbieni Bwana nchi yote, wahubirini mataifa habari za utukufu wake
na watu wote habari za maajabu yake
2. Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana, na wakuhofiwa kuliko miungu yote,
maana miungu yote ya watu si kitu, lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu
3. Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, mpeni utukufu na nguvu, mpeni Bwana utukufu wa jina lake,
leteni sadaka mkaziingie nyua zake
4. Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu, tetemekeni mbele zake nchi yote, semeni katika mataifa,
Mungu ni mfalme, atawahukumu watu kwa adili