Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 280 | Umetazamwa mara 1,298
Download NotaUpepo upepo unavuma kote duniani, {unavuma kama kimbunga (kimbunga) hofu imetanda (imetanda) miti inang'olewa nakutupwa huku na kule x2.} ni upepo wa imani unavuma kote dunia, unavuruga watu ona wanatangatanga x2.
1.Makanisa yanaongezeka duniani, wachungaji nao manabii wauongo nao ni wengi, usiposimama imara, kuilinda imani yako upepo utakapovuma utakuvuruga.
2.Wapo watu wanayaanzisha makanisa, wala sio kwa imani bali wajikimu kimaisha, usiposimama imara, kuilinda imani yako, upepo utakapovuma utakuvuruga.
3.Wakristu wakimbilia penye miujiza, hawajui yatendekayo bila kibali chake Mungu, usiposimama imara, kuilinda imani yako upepo utakapovuma utakuvuruga.