Maneno ya wimbo
Kiitikio: Ee Bwana fadhili zao na za milele, usiziache kazi za mikono yako, usiziache kazi za mikono yako usiziache kazi za mikono yako.
1.Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,mbele ya miungu nitakuimbia zaburi, na nitasujudu nikilikabili, hekalu lako takatifu.
2.Nitalishukuru jina lako Mwenyezi kwa zako fadhili pia uaminifu wako, kwa maana umekuza ahadi zako kuliko jina lako Bwana.
3.Ingawa Mwenyezi Mungu yuko mbinguni amwangalia mnyenyekevu kwa wema naye amjua mwenye kujivuna, timiza mambo yote Mungu.
4. Nilipokuita wewe ukaniitikia, ukanifariji nafsi ukanitia nguvu, fadhili zako Bwana ni za milele usisahau kazi zako.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu