Ingia / Jisajili

Hayupo Hapa Amefufuka

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Pasaka

Umepakiwa na: Valentine Ndege

Umepakuliwa mara 666 | Umetazamwa mara 1,978

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Furaha chereko pia vifijo pande zote vyasikika nderemo shangwe kinanda nazo ngoma midundo mitamu ni furaha Bwana Yesu amefufuka leo ni furaha. KIITIKIO: Hayupo hapa hayupo hapa x2 (Kumbukeni) maneno aliyowaambia aiye (Kumbukeni) maneno aliyowaambia aiye (kumbukeni) maneno aliyowaambia aiye (mauti ameyashinda kuzimu kimya kuzimu kimya hakika Bwana) amefufuka ameyashinda mauti (hakika) Bwana ameyashinda mauti x2 1. Walinzi walipewa fedha waseme Bwana Yesu hajafufuka mitume wamemuiba uongo kabuli li wazi Bwana hayumo amefufuka Aleluya. 2. Mariam na wenzake walikuta kaburi kaburi liwazi na jiwe limevilingishwa pembeni, Malaika akawaambia mnayemtafuta hayupo hapa kafufuka. 3. Nyimbo nzuri tuimbe tumwimbie Mwokozi, vigelegele na makofi tumshangilie Mwokozi hakika ametukomboa utumwa utumwa utumwa wa shetani. HITIMISHO: Shangwe shangwe shangwe ae Mkombozi wetu Bwana Yesu amefufuka aiye (Organ) Tupige kinanda ngoma na zeze tuimbeni na zaburi Mwokozi tumshangilie (Organ) Tumekombolewa utumwani mwa shetanix5

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa