Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 11,051 | Umetazamwa mara 19,819
Download Nota Download MidiKiitikio:
Hiki ndicho nilichoandaa Ee Mungu wangu nakusihi ukipokee, hii ndiyo shukrani yangu,sehemu ya pato langu itokayo ndani ya mtima wangu.
Naileta mikononi mwako ambapo nondo hawataiharibu (kwa kutu),naileta mikononi mwako ambapo mwizi hawezi kuiba, ninaileta mahali salama iwe hazina yangu mbinguni
Mashairi:
1. Ninakutolea moyo wangu,wala si mifuko yangu, ndiyo kazi ya mikono yangu nakusihi uibariki.
2.Hata kama ni kidogo nakusihi ukipokee,kwani ndicho nilichoandaa kukutolea Ee Mungu wangu
3.Hiki ninachokutolea kikakupendeze Mungu wangu, kama ile sadaka ya mtumishi wako,mtumishi wako Abeli.