Ingia / Jisajili

Maisha Mapya Katika Kristo

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Pasaka

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 1,234 | Umetazamwa mara 4,843

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo yatafuteni yaliyo juu aliko Kristo, yatafuteni yaliyo juu aliko Kristo.

Mashairi: (version ii of "Basi Mkiwa Mmefufuliwa Pamoja na Kristo")

1. Yatafuteni yaliyo juu aliko Kristo, yatafuteni yaliyo juu aliko Kristo,ameketi mkono wa kuume mkono wa kuume wa Mungu, ameketi mkono wa kuume mkono wa kuume wa Mungu.

2.Yafikirini yaliyo juu, si yale yaliyo katika nchi, kwa maana mlikufa na uhai wenu umefichwa, umefichwa pamoja na Yesu Kristo katika Mungu, umefichwa pamoja na Yesu Kristo katika Mungu.

3.Kristo atakapofunuliwa aliye uhai wetu, Kristo atakapofunuliwa aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye, mtafunuliwa pamoja naye katika utukudu.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa