Ingia / Jisajili

Hongera Fr Felix Jabu

Mtunzi: Michael Mgalatia Jelas Nkana
> Tazama Nyimbo nyingine za Michael Mgalatia Jelas Nkana

Makundi Nyimbo: Miito

Umepakiwa na: Michael Nkana

Umepakuliwa mara 478 | Umetazamwa mara 2,319

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio

Baba Mpya wa kiroho Felix Jabu Hongera Baba hongera,

Kufikia daraja hilo takatifu Hongera Baba hongera,

Umeitikia vema wito wa Mungu mwenyezi Hongera Baba Hongera

kwenda kuwa mtendaji katika shamba lake hongera Baba hongera,

//:Watawa wanakupa hongera, waimbaji tunakupa hongera watu wote wanakupa hongera sana Hongera://

Mashairi

1. Umeteuliwa na Mungu kuwachunga kondoo wake wachunge vema asipotee hata mmoja.

2.Neno la Mungu siku zote daime liwe ngao yako katika mapambano dhidi ya ibilisi.

3. Pongezi kwa wanashirika watawa wa roho mtakatifu, hongera sana kwa kumpata mtawa mpya.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa