Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,809 | Umetazamwa mara 7,147
Download Nota Download MidiKiitikio:
Nimeuona wema wa Mungu (x 2). Nimeushuhudia (mimi) maishani mwangu, na sasa ninakiri, nakiri kwenu nyote ya kwamba Mungu wetu ni mwema sana
Mashairi:
1.Nimeuona wema wa Mungu, nimeuonja wema wa Mungu, nimeushuhudia ukarimu wake, nimeyashuhudia matendo yake, leo nakiri kwamba Mungu wetu ni mwema
2.Nimeziona baraka zake, nimeuona ukarimu wake, nimeuonja upendo wake , nimeziona shuhuda zake, leo nakiri kwamba Mungu wetu ni mwema.
3. Nimejawa na furaha na amani tele, nimejawa upendo na matumaini, nina amani tele ndani ya Mungu wangu, ninafuraha kubwa isiyo kifani, leo nakiri kwamba Mungu wetu ni mwema.