Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,601 | Umetazamwa mara 4,893
Download NotaKiitikio:
Natamani kujongea mezani pako ili nishiriki karamuyo nishiriki na wenzangu, nakusihi nipokee mezani pako nile mwili wako pia ninywe damu yako x2 //
Mashairi
1. Meza yako e bwana ni meza ya amani, meza ya upatanisho meza yako ni ya ukarimu
2. Meza yako e bwana ni meza ya furaha ndiyo meza ya amani tulizo la nafsi zetu
3.Meza yako e bwana ni meza ya faraja ndiyo meza ya amani tulizo la nafsi zetu
4. Meza yako e bwana ni meza ya amani yatupatanisha sote kwa mwili na damuyo.