Maneno ya wimbo
MTAKATIFU SESILIA
(Sop): Mtakatifu Sesilia
(All): msimamizi, msaada,mwombezi wa waimbaji wote
(Bass: ewe Sesilia) twakufurahia ee mama twakushangilia,
(Bas/Tenor: Sesilia) twakufurahia ee mama twakushangilia
1. Tujalie upole wako ee mama Sesilia, ili nasi tuwe wapole tukuige
wewe tuzifuate amri maagizo ya Mungu, tuwe kielelezo chema
kwa wenzetu wote
2. Tuombee kwake Mwenyezi ee mama Sesilia, atujaze neema zake
na Baraka yake, tuvihistahimili vishawishi vya dhambi, tuwe na
imani dhabiti kwake Mungu Baba
3. Tujalie tujitolee kwa wenzetu wote, kama ulivyojitolea maishani
mwako, tuwahubirie injili ya Bwana kwa nyimbo zetu na hasa
kwa matendo yetu mema
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu