Ingia / Jisajili

Natamani Kuijongea Meza yako

Mtunzi: Gabriel N. Kimani
> Mfahamu Zaidi Gabriel N. Kimani
> Tazama Nyimbo nyingine za Gabriel N. Kimani

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Gabriel Kimani

Umepakuliwa mara 199 | Umetazamwa mara 899

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
NATAMANI Natamani kuijongea meza yako Bwana Nijiunge nao wenzangu wanao kupokea Lakini siwezi, siwezi, siwezi, siwezi mimi siwezi siwezi bila msaada wako siwezi mimi siwezi. 1. Moyo wangu Bwana wakuonea shauku, nataka kuja hapo ulipo nikupokee, lakini naona haya, Bwana kwani moyo wangu umejaa dhambi. 2. Natazama wenzangu wanao kupokea wanajongea altare yako kwa madaha, sijui nifanye nini, Bwana kwani dhambi zangu zinanizuia. 3. Bwana wangu naomba jambo moja kwako nalo ndilo msamaha wako ewe Bwana niweze kukupokea Bwana ili uje ndani ya moyo wangu. 4. Nakusihi uingiapo ndani yangu, niumbe upya Bwana niwe kiumbe chako, uniongoze daima, Bwana nisije tena nikaanguka dhambini.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa