Maneno ya wimbo
TUONGOZE MAMA
Tuangazie njia Mama tufike makao ya uzima makao ya uzima X2
Giza ni totoro limeyafunika macho yetu ee mama (twapotea)
twahitaji msaada wako mama (Maria) njoo mama njoo mama njoo
mama utuongoze twpotea njia X2
1. Twakukimbilia Maria, Bikira mwenye huruma tutie nguvu ya
safari tufike kwa mwanao Yesu Kristu.
2 Safari ni ndefu Maria, shetani atusumbua hatua ni nzito Maria
miguu yetu imelegea.
3. Utupe nguvu ee Maria, tusije vunjika moyo, tuwe shupavu na
imara katika safari hii ya kiroho.
4. Utuombee kwa mwanao atujaze ujasiri , tuweze kumshinda
shetani tuweze kufika huko mbinguni
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu