Ingia / Jisajili

Nikitazama Pande zote

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Valentine Ndege

Umepakuliwa mara 381 | Umetazamwa mara 1,544

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Nikitazama pande zote pande zote za dunia nikitazama Mashariki nikitazama Magharibi Kaskazini nako Kusini nauona ukuu wako Mungu wangu x2 Tunakurudishia sifa heshima na utukufu wewe unayeketi juu ya makerubi uhimidiwe milele upewe sifa milele yote x2 1. Itazame mimea makondeni inavyochanua inavyopendeza yapendeza, ni wewe Mungu ulipenda kuipamba dunia uhimidiwe milele. 2. Watazame wanyama wa mwituni wanavyopendeza wanavyokusifu Mungu wao, ni wewe Mungu ulipenda kuipamba dunia uhimidiwe milele. 3. Waoneni samaki baharini wanashangilia ukuu wa Mungu Muumba wao, ni wewe Mungu ulipenda kuipamba dunia uhimidiwe milele. 4. Itazame milima na mabonde yanavyovutia uso wa dunia wa dunia, ni wewe Mungu ulipenda kuipamba dunia uhimidiwe milele

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa