Ingia / Jisajili

Ninakuungamia

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Mika Wihuba

Umepakuliwa mara 445 | Umetazamwa mara 1,469

Download Nota
Maneno ya wimbo

Ninakuungamia, Mungu wangu, nimekosa ninapiga magoti kwa unyenyekevu uniwie radhi mimi mdhambi, Ninayakili wazi, maasi  yangu, kwako Bwana ninapiga kifua nikiomba toba kwa machozi na kwa kuomboleza, (Katika unyonge wangu ninakulilia usikie, sauti, yakuomba kwangu Bwana wangu, unihurumie unisamehe x2).

  • 1.Nayatubu makosa yangu yote, mbele yako Mungu wangu, kwa yote niliyokutendea wewe, najirani zangu.
  • 2.Msamaha wako ndiyo kitulizo changu, uyafute makosa yangu, unifanye mtu mwema mtu mwema, unifanye mtu mwema.
  • 3.Huruma yako, Bwana na rehema zako, zinifanye nikuelekee, nikuelekee wewe daima, niufikie uzima wa milele.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa