Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 5,831 | Umetazamwa mara 10,730
Download Nota
Kiitikio:
Njoni mpate neema tele neema za Ki-Mungu, njoni mpate faraja kutoka mbinguni (x2)
Njoni mzipokee baraka toka kwa Mungu (njoni) njoni muonje upendo ulio wa kweli
Mashairi:
1. Ndugu usisite hebu njoo mbele zake umweleze shida zako atakusikiliza.
2. Njoo, njoo, njoo kwa Bwana, njoo na mizigo ya dhambi zako naye ataitua.
3.Bwana akuita (ili aweze) aweze kukusaidia akupatie baraka zake zote ili ubarikiwe.
4. Bwana ni mwema kwa watu wote wanaomuhitaji, Bwana yu karibu na wale wote wamuitao.