Ingia / Jisajili

Njooni Tuwashuhudie

Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa

Makundi Nyimbo: Ndoa

Umepakiwa na: Nivard Silvester

Umepakuliwa mara 1,606 | Umetazamwa mara 2,919

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Shairi: 1. Mikononi wameshikana, ona wanaandamana, pendo kuhakikishiana, hekaluni wanaingia. Kiitikio: Njooni njooni njooni, njooni wake kwa waume, njooni tuwashuhudie wapendwa wanavyoungana. Mashairi mengine: 2. Tangu walipovutiana, nia waliwekeana, siku moja waje ungana, leo wanatimiziana. 3. Safari ndefu tena ngumu, leo yaishia humu, wanavalishwa majukumu, kuunda kizazi timamu. 4. Sisi tutawashuhudia, wao waahidiana, Mwenyezi ataunganisha, ndoa yao kukamilika. 5. Chereko, nderemo vifijo, vitoke ndani ya moyo, Mwenyezi atukuzwe humo, daima milele milele.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa