Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 725 | Umetazamwa mara 2,104
Download Nota Download MidiSasa ni wakati wakupeleka sadaka kwa Bwana kama Shukrani kwa mema anayotujalia.
Kiitikio:
Inuka twende tukampe Mungu wetu x2. (mazao ya shamba) Peleka (hata na mifugo) peleka (fedha mifukoni) peleka kampe Bwana.
Beti:
1.Tutungue hazina zetu tukatoe Sadaka zetu, tukamtolee Bwana Mungu wetu Sadaka.
2.Tunahangaika sana kutafuta utajiri wa Dunia, tutoe sadaka na hayo tutazidishiwa.
3.Unapotoa sadaka yako rudi kwanza ukapatane na ndugu yako ndipo ukatoe sadaka yako kwa Bwana.
4.Ee Mungu wanijua mimi ni mdhaifu, nishike mkono niokoe ulimwengu wa mateso, nakusihi ipokee sadaka yangu.