Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 4,128 | Umetazamwa mara 8,388
Download Nota Download Midi
Kiitikio:
Nitatangaza sifa zako muda wote ningali hai, nitahubiri matendo yako bila kuchoka, sitasita kuyashuhudia uliyonitendea. Sitanyamaza, sitanyamaza kuzitangaza sifa zako, sitanyamaza daima kuyanena makuu uonitendea, sitachoka kuzitangaza sifa zako.
Mashairi:
1.Usiku na mchana nitamsifu bila kuchoka, mbele ya mataifa nitalisifu jina lake.
2. Maana wema wake kwangu umekuwa bila wa mipaka, huruma zake kwangu hazihesabiki machoni pake.
3.Nitazitangaza sifa zake watu wote wapate kumjua, nitazihubiri sifa zake watu wote wapate kumjua, kamwe sitachoka kumtangaza ningali hai.