Mtunzi: Joseph Rimisho
> Mfahamu Zaidi Joseph Rimisho
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Rimisho
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: JOSEPH RIMISHO
Umepakuliwa mara 1,777 | Umetazamwa mara 4,148
Download Nota Download MidiKiitikio
Siku ile niliyokuita uliniitikia, ukanifariji nafsi yangu kwa kunitia nguvu.X2
Mashairi
1.Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, mbele ya miungu nitakuimbia zaburi, nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu.
2.Nitalishukuru jina lako,kwa ajili ya fadhili na uaminifu wako, kwa maana umekuza ahadi yako kuliko jina lako.
3.Bwana yuko juu amwona mwenye haki, naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali, nijapokwenda kati ya shida wewe utanihuisha.
4.Bwana atanitimiliza mambo yangu, ee Bwana fadhili zako ni za milele, usiziache kazi za mikono kazi za mikono yako.