Mtunzi: John Keneddy Kizza
> Mfahamu Zaidi John Keneddy Kizza
> Tazama Nyimbo nyingine za John Keneddy Kizza
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Keneddy Kizza
Umepakuliwa mara 871 | Umetazamwa mara 2,754
Download Nota Download Midi
Simameni tujongee, mbele zake Bwana Yesu kwa mwili na damu yake, twende wote tushiriki X2
(Yesu) ameandaa chakula, chenye uzima wa milele, jongeeni enyi wakristu, Bwana Yesu atushibishe X2
1. Yesu ndiye chakula na kinywaji toka mbinguni, atuita tukampokee ili tuwe na uzima.
2. katika mwili wake Yesu, pia na damu yake Kristu, kuna uzima wa milele na baraka za mbinguni.
3. Hakika Bwana mkarimu atuunganisha mezani, kweli yeye ni mwenye upendo utokao mbinguni.
4. Enyi wenye mioyo safi jongeeni kwenye chakuula, pokeeni kwa heshima kuu yumo ndani ya Ekaristi.
5. Wale wote wanayo heri wanaokaribia kwake, wataishi naye siku zote, hawatakufa daima.