Mtunzi: John Keneddy Kizza
> Mfahamu Zaidi John Keneddy Kizza
> Tazama Nyimbo nyingine za John Keneddy Kizza
Makundi Nyimbo: Noeli | Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Keneddy Kizza
Umepakuliwa mara 986 | Umetazamwa mara 2,371
Download Nota Download MidiTUMTOLEE AMEZALIWA LEO
(Kwa shangwe tutoe zawadi) kwa Mungu aliyezaliwa kwa furaha na shangwe tumwimbie (tushike zawadi) tena kwa furaha na shangwe tumtolee Mwokozi wetu amezaliwa leo. X2
1. Tutoe zawadi za kumpendeza za ubani na dhahabu kwa Mwokozi aliyezaliwa tumpe heshima, tumpe heshima.
2. Mamajusi nao wakamtolea mtoto zawadi wakafunguwa hazina zao kumsujudia, tumpe heshima.
3. Tukongozwa na sauti tamu Malaika wanaimba tumtazame Mfalme wa mbingu amezaliwa, tumpe heshima.
4. Atapokea matoleo yetu tukitoa kwa dhati ndiye Mungu wa mbingu na nchi atatubariki tumpe heshima.