Maneno ya wimbo
UTUKUFU KWA MUNGU JUU
(Misa Ya Mashahidi Wa Uganda)
Kitikio
Utukufu kwa Mungu, utukufu kwa Mungu juu mbinguni.
Na amani (pote!) duniani (kweli!), kwa watu wenye mapenzi mema.
Mashairi
1. Tunakusifu, tunakubariki, tunakuabudu, tunakutukuza.
Tunakushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu, Ee Bwana Mungu,
Mfalme wa mbinguni, Mungu baba, Ee Mungu Baba mwenyezi’
2. Ee Bwana Yesu Kristo, Mwana wa pekee, Mwanakondoo wa Mungu .
Uondoaye dhambi za dunia , utuhurumie.
Uondoaye dhambi za dunia , pokea ombi letu.
3. Ewe mwenye kuketi kuume kwa Baba, utuhurumie.
Kwakuwa ndiwe uliye peke yako Mtakatifu, Ee Bwana Yesu,
kwakuwa ndiwe uliye peke yako Mkuu, Yesu Kristo.
4. Pamoja na Roho Mtakatifu
katika utukufu wa Mungu Baba mwenyezi,
Amina, Amina.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu