Mtunzi: Emmanuel Daniel Mutura
> Tazama Nyimbo nyingine za Emmanuel Daniel Mutura
Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari | Mwaka wa Huruma ya Mungu
Umepakiwa na: Emmanuel Daniel Mutura
Umepakuliwa mara 330 | Umetazamwa mara 1,279
Download NotaTUMEKOSEANA (SISI TU WAKOSEFU) - E.D.MUTURA
1. Tumekoseana na wenzetu wa ndoa, tuna majeraha mengi mioyoni mwetu; tumekoseana na majirani zetu, tuna majeraha mengi mioyoni mwetu:
Kiitikio:
Ili kuomba huruma ya Mungu tupeane mikono tutembee pamoja tufungue vifungo vifungo vya dhambi zetu, kwa unyenyekevu twende, mbele zake Mungu kuomba huruma yake. Tujipatanishe na Mungu na wenzetu, kwa unyenyekevu twende, mbele zake Mungu kuomba huruma yake.
2. Tumefarakana na wazazi wetu, tuna majeraha mengi mioyoni mwetu; tumefarakana na watoto wetu, tuna majeraha mengi mioyoni mwetu:
3. Tumekwaruzana na wanakwaya wenzetu, tuna majeraha mengi mioyoni mwetu; tumekwaruzana na wachungaji wetu, tuna majeraha mengi mioyoni mwetu:
4. Tumesengenyana na wafanyakazi wenzetu, tuna majeraha mengi mioyoni mwetu; tumesengenyana na viongozi wetu, tuna majeraha mengi mioyoni mwetu:
Hitimisho:
Sisi tu wakosefu, Baba tuhurumie.