Ingia / Jisajili

Kuna Furaha Katika Kutoa

Mtunzi: Emmanuel Daniel Mutura
> Tazama Nyimbo nyingine za Emmanuel Daniel Mutura

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Emmanuel Daniel Mutura

Umepakuliwa mara 625 | Umetazamwa mara 1,757

Download Nota
Maneno ya wimbo

KUNA FURAHA KATIKA KUTOA [E.D.MUTURA]

(Inukeni Twende Tukatoe)

Inukeni twende tukatoe michango yetu (waamini) inuka twende bila ya kusitasita (tuwe wakarimu) kwani kuna furaha tena kuna furaha furaha kubwa sana kumtolea Mungu wetu; pia tunapokea pia tunapokea baraka nyingi sana tukimtolea kwa moyo.

  1. Toa ndugu yangu kwa ukarimu, toa bila ya manung'uniko, hakika nawe ndugu utabarikiwa.
  2. Ni furaha kubwa katika kutoa, ni furaha katika kutoa, toa kwa moyo wote upate furaha.
  3. Kwa kumtolea Mungu pato lako, Yeye mtoa wa mapaji yote, hakika atakupa baraka na neema.
  4. Mjaribu Mungu katika kutoa, hapo ndipo utakaposhangaa, kuziona baraka zikimiminika.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa