Ingia / Jisajili

Tunakutukuza

Mtunzi: Martin Mutua Munywoki
> Tazama Nyimbo nyingine za Martin Mutua Munywoki

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani

Umepakiwa na: Martin Munywoki

Umepakuliwa mara 437 | Umetazamwa mara 1,391

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
T U N A K U T U K U Z A @Martin Munywoki 1. Pande zote za dunia, viumbe wako wote wakushangilia, Watu wanakuinua, nasi tunakuimbia; Umekuwa mwaminifu, watukumbuka sisi tulio dhaifu, Tusojua kukusifu, wewe mwenye utukufu. Kwa zeze na vinanda - tunakutukuza Baragumu na panda - tunakutukuza Nderemo zimetanda - tunakutukuza Na ngoma zinadunda - tunakutukuza Iyee (ae hoye) , aiyee (ae hoye ) aiyee (ae hoye) tunakutukuza Aiyee (ae hoye) , aiyee (ae hoye ) aiyee (ae hoye) tunakutukuza 2. Sina budi kushukuru, ulinivua giza kanivika nuru, Utumwa kaninusuru, kaniweka niwe huru; Japo mimi hukosea, hujanitupa bado wanihurumia, Hata ninapopotea, wanielekeza njia. Kwa nyimbo na zaburi - tunakutukuza Filimbi na zumari - tunakutukuza Kayamba na matari - tunakutukuza Na kwa sauti nzuri - tunakutukuza 3. Unipaye bure hewa, kunitetea kila ninapoonewa, Kwako sijapungukiwa, wala sijaelemewa; Unayenipa mkate, na kunilinda kote wakati wowote, Nijalie nisisite, kukusifu siku zote. Sifa zote ni zako - tunakutukuza Huko juu uliko - tunakutukuza Vigelegele, heko - tunakutukuza Na shangwe na chereko - tunakutukuza * * * Una neema tele - tunakutukuza Tangu enzi za kale - tunakutukuza Na umebaki vile - tunakutukuza Milele na milele - tunakutukuza Wasio na chakula - unawapokea Wasona pa kulala - unawapokea Wajapo kwako bila - unawapokea Unawajibu sala - unawapokea * * * Vipofu wanaona - wanakutukuza Viwete wanapona - wanakutukuza Tasa wapata mwana - wanakutukuza Na bubu wananena - wanakutukuza Kweli wewe ni baba - tunakutukuza Daima watubeba - tunakutukuza Kwako twapata tiba - tunakutukuza Watukinga misiba - tunakutukuza

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa