Ingia / Jisajili

Chakula Cha Watoto

Mtunzi: Martin Mutua Munywoki
> Tazama Nyimbo nyingine za Martin Mutua Munywoki

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Martin Munywoki

Umepakuliwa mara 797 | Umetazamwa mara 3,371

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Si sawa kuchukua chakula cha watoto (si sawa) 

Na kuwatupia mbwa chakula cha watoto (lakini)

Hata mbwa hula makombo yaangukayo (kutoka) mezani mwa Bwana wao

Nami natamani kuonja chakula hiki  (ulicho) waandalia wanao

{ Japo sifai mimi nakusihi Yesu, uniruhusu } *2

1. Ninatamani sana, Bwana wangu (mwema), kujongea karamuni,

Ijapokuwa mimi sina moyo safi, nina njaa nina kiu kukupokea

   
3. Ninapokupokea, mwili wako (Bwana), nina uzima milele
Sasa niende wapi zaidi ya kwako, nisamehe niruhusu nikupokee
 
4. Kwa kuwa ulikuja, duniani (kwao), wenye dhambi kama mimi
Ulikula nao hata ukafa nao, nami leo nasogea nikupokee
 


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa