Mtunzi: Martin Mutua Munywoki
> Tazama Nyimbo nyingine za Martin Mutua Munywoki
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Martin Munywoki
Umepakuliwa mara 601 | Umetazamwa mara 2,292
Download Nota Download MidiTuvumiliane tuvumiliane, tuishi kwa upendo nao wenzetu
Tuwakubali hao jinsi walivyo, ijapokuwa hawafanani nasi
1. Wapo walio masikini wahitaji, miongoni mwetu
Tusiwachoke wanapoombaomba, tuwavumilie
Wengine hawana elimu kama sisi, miongoni mwetu
Tuwaeleze kwa upole na pia, tuwavumilie hivyo
2. Wengine wa asili tofauti nasi, miongoni mwetu
Tusizidharau tamaduni zao, tuwavumilie
Pia wapo wengi wa dini mbali mbali, miongoni mwetu
Tusiwahukumu kwa imani yao, tuwavumilie hivyo
3. Malezi na mapito yetu sio sawa, miongoni mwetu
Wengine wameona machungu mengi, tuwavumilie
Wengine hukasirika haraka sana, miongoni mwetu
Tusiwe sababu ya machozi yao, tuwavumilie hivyo