Ingia / Jisajili

Tunu Za Kikristo

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 2,253 | Umetazamwa mara 5,836

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Upendo na amani ndio tunu za Kikristo, upatanisho na kutenda(kutoa) haki ndiyo msingi wa Imani yetu(x2)

Basi hatuna budi kuvienzi kwa vitendo, kuwa mfano kwa wengine kwa yote tuyafanyayo, kuwa kielelezo bora cha ukristo wetu(x2)

Mashairi:

1. Kristo alitufundisha tupendane sisi kwa sisi kwani hakuna amri kuu zaidi ya amri ya mapendo, hivyo ndugu tupendane kama Kristo alivyotupenda, upendo kwa wengine ndiyo chimbuko la Ukristo.

2. Upendo na upatanisho ndiyo chimbuko la Ukristo, ndiyo tunu za Kikristo, tunu za Kikristo.


Maoni - Toa Maoni

Pastory egid Sep 22, 2021
Kila navyojaribu kupakua hazikubali

Toa Maoni yako hapa