Mtunzi: Ernest Magunus
> Mfahamu Zaidi Ernest Magunus
> Tazama Nyimbo nyingine za Ernest Magunus
Makundi Nyimbo: Kwaresma | Zaburi
Umepakiwa na: ERNEST MAGUNUS
Umepakuliwa mara 596 | Umetazamwa mara 2,119
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Jumatano ya Majivu
- Katikati Dominika ya 1 ya Kwaresma Mwaka A
Kiitikio:
||: Uturehemu Ee Bwana, Uturehemu Ee Bwana Uturehemu Kwa kuwa tumetenda dhambi :||
1. Ee Mungu, unirehemu, sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.
2. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua Mimi makosa yangu, Na dhambi yangu I mbele yangu daima.
3. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.
4. Usinitenge na uso wako, Wala roho wako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako.
5. Unitegemeze kwa roho ya wepesi. Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kiywa changu kitazinena sifa zako.