Mtunzi: Alan Mvano
> Mfahamu Zaidi Alan Mvano
> Tazama Nyimbo nyingine za Alan Mvano
Makundi Nyimbo: Pentekoste
Umepakiwa na: Alan Mvano
Umepakuliwa mara 3,866 | Umetazamwa mara 8,906
Download Nota Download MidiKiitikio
Waipeleka roho yako Ee Bwana
Nawe waufanya upya uso wa nchi
Mashairi
1.Ee nafsi yangu umhimidi Bwana, wewe Bwana Mungu wangu, umejifanya mkuu sana
Ee Bwana jinsi yalivyo mengi matendo yako, dunia imejaa mali zako.
2.Waiondoa pumzi yao wanaokufa na kuyarudia mavumbi yao,
waipeleka roho yako, wanaumbwa, nawe waufanya upya uso wa nchi.
3.Utukufu wa Bwana na udumu milele, Bwana na ayafurahie matendo yake,
kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake, mimi nitamfurahia Bwana.