Maneno ya wimbo
YESU YUPO KATIKA EKARISTI
1. Waamini wapendwa, je, mnafahamu kwamba
katika Ekaristi anakaa Yesu Kristo?
Ndio, Bwana yupo katika mkate na divai,
mkate tunayokula na divai tunayokunywa.
Kitikio:
Yesu yumo katika mwili wake.
Yeye yumo katika damu wake.
Kristo yumo katika roho wake.
Kweli Bwana yumo katika uungu wake.
Ndio, Yesu yupo katika Ekaristi.
2. Ekaristi ni sakramenti ya upendo,
sakramenti ambayo Bwana anautoa mwili wake
na kumwaga damu yake kwa ajili yetu.
Ekaristi ni sakramenti ya upendo mkubwa.
3. Tujongee meza yake Bwana Yesu Kristo,
Sote tule mkate na sote tunywe divai.
Kwa maana katika Ekaristi
tunampokea Bwana wetu alie hai.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu