Ingia / Jisajili

Ee Bwana Mungu Wangu

Mtunzi: Thomas G. Mwakimata
> Tazama Nyimbo nyingine za Thomas G. Mwakimata

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Pasaka | Zaburi

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 1,597 | Umetazamwa mara 3,628

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 3 ya Pasaka Mwaka C

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ee Bwana Mungu wangu nalikulilia ukaniponya, Ee Bwana nalikulilia ukaniponya x 2:

Mashairi:

1 (a)  Ee Bwana nitakutukuza kwa maana umeniinua, wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.

1 (b)  Umeniinua nafsi yangu ee Bwana, nafsi yangu kutoka kuzimu.

2 (a)  Umeniuhisha na kunitoa, miongoni mwao washukao shimoni.

2 (b)  Mwimbieni Bwana, mwimbieni zaburi, enyi watauwa watauwa wake.

3 (a)  Nakufanya shukrani kwa kumbukumbu, kwa kumbukumbu la utakatifu wake.

4 (a)  Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, katika radhi yake mna uhai.

5 (a)  Huenda kilio huja kukaa usiku, lakini asubuhi huwa furaha.

3 (b)  Ee Bwana usikie unirehemu, Bwana uwe msaidizi wangu.

4 (b)  Uligeuza matanga yangu kuwa machezo, Ulinivua gunia ukanivika furaha.

5 (b)  Ee Bwana Mungu wangu ee Mungu wangu, Ee Bwana nitakushukuru milele.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa