Mtunzi: Thomas G. Mwakimata
> Tazama Nyimbo nyingine za Thomas G. Mwakimata
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Zaburi
Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata
Umepakuliwa mara 4,377 | Umetazamwa mara 8,769
Download Nota Download MidiBwana amejaa huruma na neema Bwana amejaa huruma na neema x 2:
Mashairi:
1 (a) Akusamehe maovu maovu yako yote, Bwana amejaa huruma na neema,
1 (b) Akuponya magonjwa magonjwa yako yote, Bwana amejaa huruma na neema.
2 (a) Aukomboa uhai wako na kaburi, Bwana amejaa huruma na neema,
(b) Akutia taji ya fadhili na rehema, Bwana amejaa huruma na neema.
3 (a) Bwana amejaa huruma na neema, Bwana amejaa huruma na neema,
(b) Haoni hasira upesi ni mwingi wa fadhili, Bwana amejaa huruma na neema.
4 (a) Hakututenda sawasawa na hatia zetu, Bwana amejaa huruma na neema.
(b) Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu, Bwana amejaa huruma na neema
5 (a) Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Bwana amejaa huruma na neema,
(b) Ndivyo Mungu alivyoweka dhambi zetu mbali nasi, Bwana amejaa huruma na neema.
6 (a) Kama vile Baba awahurumiavyo watoto wake, Bwana amejaa huruma na neema.
(b) Ndivyo Mungu alivyoweka dhambi zetu mbali nasi, Bwana amejaa huruma na neema.