Ingia / Jisajili

Ingekuwa Heri Leo

Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Alfred Ogombo

Umepakuliwa mara 595 | Umetazamwa mara 1,825

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 23 Mwaka A

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ingekuwa ingekuwa heri, leo msikie sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu, Ingekuwa heri leo, msikie sauti yake x2

1.Njoni tumwimbie Bwana, na tumfanyie shangwe mwamba, mwamba wa wokovu wetu

2.Tuje mbele zake Bwana, tuje kwa shukrani tumfanyie, tumfanyie shangwe kwa zaburi

3.Njoni tuabudu Bwana, tusujudu tupige magoti, mbele za  ke Muumba wetu

4.Ndiye Mungu wetu nasi, tu watu wa malisho yake, na kondoo za mkono wake

5.Msifanye migumu mioyo, mlivyofanya kule Meriba, kama siku ya Masa jangwani

6.Hapo walinijaribu, baba zenu na wakanipima, wakayaona matendo yangu


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa