Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Ndoa
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 1,394 | Umetazamwa mara 3,677
Download Nota Download MidiMungu ubariki hii ndoa ya wenzetu (Njoo bwana harusi na bibi harusi) mpate baraka kutoka kwa Mungu Baba (baraka mpate) na muishi mkipendana siku zote
1.Mungu awajalie baraka za uzazi,
na watoto wenu muwatunze vema
wawe watiifu ndio wampendeze Mungu
2.Mungu awajilie pia maisha bora,
mapato yenu yakidhi mahitaji
Bwana ndiye Mpaji kamwe kitu hamtakosa
3.Muwe mfano bora kwa majirani zenu,
muige familia ile takatifu
ya Maria Yosefu na Bwana wetu Yesu
4.Tunawatakia afya njema siku zote,
maisha marefu Mungu 'wajalie
baraka neema ziwe nanyi siku zote