Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Miito
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 607 | Umetazamwa mara 2,424
Download Nota Download Midi1.Hekima nguvu roho akukabidhi, siku zote ukahubiri neno
Ujasiri uwezo neema akupa, siku zote ukahubiri neno
Nenda uhubiri hili neno jema, kote kwao mataifa mbalimbali
Ulimwenguni kote ulitangaze, ulitangaze hili neno jema
2.Nenda ulimwenguni ukawafanye, mataifa yote kuwa wafuasi
Uwabatize kwa jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu
3.Uwafundishe mambo hayo yote, ambayo Bwana amekuamuru
Hakika yuko pamoja nawe siku, zote hadi mwisho wa dahari
4.Bwana amekutuma kama kondoo, aliye katikati ya mbwa mwitu
Kwa hiyo uwe mwerevu kama nyoka, tena uwe mpole kama hua