Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 2,168 | Umetazamwa mara 5,585
Download Nota Download Midi[Bwana ndiye mchungaji (Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu) x2] x2
1.Kwenye malisho ya majani, kwenye malisho ya majani mabichi hunilaza,
kando ya maji matulivu - kando ya maji matulivu huniongoza
2.Hunihuisha nafsi yangu, hunihuisha nafsi yangu na kuniongoza,
katika njia za haki - katika njia za haki kwa’jili ya jina lake
3.Naam nijapopita kati, ya bonde la uvuli wa mauti sitaogopa,
mabaya Wewe u pamoja nami - gongo lako na fimbo yako vyanifariji
4.Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu wanipaka mafuta,
umenipaka mafuta – kichwani pangu na kikombe changu kinafurika
5.Hakika wema na fadhili, zitanifuata siku zote za maisha yangu,
nami nitakaa nyumbani - nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele