Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Pentekoste
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 2,616 | Umetazamwa mara 9,398
Download Nota Download Midi1.Uje Roho Muumbaji utazame, roho zetu
Jaza neema za mbinguni, ndani ya viumbe vyako
2.Unaitwa Mfariji paji lake, ’liye juu
Chemchemi ya uzima moto, pendo mpako wa rohoni
3.Mtoa wa vipaji saba na kidole, chake Mungu
Mwahidiwa naye Baba, na msemesha ndimi zetu
4.Tia nuru akilini na upendo, mioyoni
Tegemeza miili yetu, kwa imara ya kudumu
5.Ufukuze pepo mbali na amani, tupe hima
Hivyo uwe kiongozi, tuepuke ovu lote
6.Umjulishe kwetu Baba tukamjue, pia Mwana
Tukakusadiki Wewe, Roho utokaye kwao
7.Atukuzwe Mungu Baba na Mwanawe, mfufuka
Pia Roho Mtakatifu, kwa milele na milele. Amina