Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 1,123 | Umetazamwa mara 3,041
Download Nota Download Midi1.Bwana ametualika kwa karamu takatifu,
tujongee ametuandalia chakula
Kimeandaliwa leo kwa ajili yetu sisi,
wanadamu tule tujaliwe wokovu
Tule mwili wake Bwana ni chakula cha uzima twende ndugu twende
Tunywe damu yake Bwana ni kinywaji cha uzima twende ndugu twende
2.Nasi tumetunukiwa tuzo hilo la milele,
heri yetu tumeandaliwa karamu
Neema tunazipata roho zetu zinaponywa,
tunaimarika katika nyoyo zetu
3.Cheo zetu na mamlaka heshima tunayopewa,
mbele zake Mungu sisi sote ni sawa
Hivyo yatupasa sote tunyenyekee mbele zake,
ndiye ametujalia haya maisha
4.Heri yetu heri yetu tuliyoitika wito,
wa kushiriki kwenye karamu ya Bwana
Tuepukane na dhambi tutende yaliyo mema,
hapo ndipo tutamfurahisha Mwenyezi