Ingia / Jisajili

Asante Tupu

Mtunzi: Wachira Sammy
> Mfahamu Zaidi Wachira Sammy
> Tazama Nyimbo nyingine za Wachira Sammy

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Samuel wachira

Umepakuliwa mara 143 | Umetazamwa mara 220

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
1. Ninakushukuru Mungu wangu Muumba wa vitu vyote vilivyomo duniani na vilivyo Mbinguni Neema zako zinanitosha tazama navyopendeza jinsi ulivyoniumba nasema asante sana Nitakuimbia Mungu wangu na kuzitangaza sifa zako ee Mungu Mwenyezi (Pokea sifa zote (Baba) ee Mungu wangu enzi na utukufu ni zako milele)X2 (Nasema asante tupu asante tu ee Baba asante sana asante tu) X2 2. Umenijalia afya njema ee Mungu wangu, maisha yangu umeyapamba upendo wako Najivunia furaha yako ee Mungu wangu nitakuimbia Mungu wangu milele yote. 3. Sina kitu cha kujivunia Mwokozi wangu ila upendo wako ee Baba na huruma yako Nikushukuruje Mungu wangu kwa ukarimu na huruma yako nyingi sana ee Baba yangu 4. Uligeuza kilio changu kuwa kicheko ukanifuta machozi yangu nilipokuita Uso wangu umeung’arisha kwa pendo lako nitakuimbia kwa vinubi hata na vinanda

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa