Mtunzi: Wachira Sammy
> Mfahamu Zaidi Wachira Sammy
> Tazama Nyimbo nyingine za Wachira Sammy
Makundi Nyimbo: Ndoa
Umepakiwa na: Samuel wachira
Umepakuliwa mara 5,018 | Umetazamwa mara 9,629
Download Nota Download Midi1. Barua nimekuandikia mpenzi tulia uisome
Miaka sasa inasogea sina budi
kukuarifia
Inatupasa kuliwazia jambo hili la
kufunga ndoa
Twende kanisani tukapate Baraka
zake Mungu mwenyezi
Chorus : Nimeamua ni wewe pekee mpenzi wangu sina
mwingine
Nimekubali kukupokea mpenzi
wangu nivishe pete
Mpenzi njoo tuandamane
Pingu za maisha tuzifunge
Pokea pete hii ni ishara
Ya upendo wangu kwako wewe
(Kwa jina la Baba na la mwana Roho
mtakatifu Amina) x2
2. Nikitazama jinsi wenzangu
wanavyojongea altareni
Moyo wangu unahuzunika ninapowazia jambo hili
Inatupasa kuishiriki sakramenti hii ya upendo
Tusiwe tu wa kushangilia kwenye harusi za wenzi wetu
3. Ni wengi wamenitamania niweze fungua
roho kwao
Najua kwako ni vilevile wengi wanakumezea mate
Wakati sasa umeshafika mpenzi njoo tuweke wazi
Ulimwengu wote utambue mimi nawe kweli twapendana