Ingia / Jisajili

Sauti ya Mtu Nyikani

Mtunzi: Wachira Sammy
> Mfahamu Zaidi Wachira Sammy
> Tazama Nyimbo nyingine za Wachira Sammy

Makundi Nyimbo: Majilio

Umepakiwa na: Samuel wachira

Umepakuliwa mara 865 | Umetazamwa mara 3,279

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

SAUTI YA MTU NYIKANI

Yohane kahubiri na kusema, kama ilivyoandikwa na Isaya.  Sauti ya mtu aliaye nyikani, tayarisheni njia njia yake Bwana, itengenezeni njia njia yake Bwana sawazisheni vilima mabonde yanyoshwe. (Tubuni tubuni sasa ufalme wakaribia onyesheni kwa vitendo ya kwamba mmetubu x2

1.      Enyi kizazi cha nyoka nani aliyesema muikimbie ghadhabu, ghadhabu inayokuja,

 (onyesheni kwa vitendo) ya kwamba mmetubu.

 

2.      Msijisemee sasa baba yetu Abrahamu nawaambieni hakika Mungu wenu anawaweza, (kuyafanya mawe haya) yakawa watoto wake.

 

3.      Shoka lake li tayari kwenye mizizi ya miti isiyozaa matunda matunda yale mazuri, (Itakatwa na kutupwa) kutupwa katika moto.

 

4.      Yohane akawaambia aliye na nguo mbili amgawiye na yule yule asiye na nguo, (Na aliye na chakula) naye pia vilevile.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa