Mtunzi: Reuben Maghembe
> Tazama Nyimbo nyingine za Reuben Maghembe
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Kwaresma | Mazishi
Umepakiwa na: Reuben Maghembe
Umepakuliwa mara 1,258 | Umetazamwa mara 2,976
Download Nota Download MidiITIKIO
Bwana
nakuhitaji wewe katika maisha yangu (wewe) *2
Katika
mateso haya ya ulimwengu (nakuomba uje uniokoe)
Bwana
Mungu uje unikoe Bwana *2
BETI
1.
Ee Mungu wangu nimezungukwa na mawimbi ya wovu, na maisha ya mateso na dhiki,
nahitaji mkono wako nipate kuokolewa
2.
Ee Mungu wangu ulimwengu huu umejaa vita, na mambano ya mali na maasi, mauaji
ya wanyonge nayo yamepamba moto
3.
Ee Mungu wangu,haya maisha ya sasa ni ya hofu, maovu yamekuwa ndiyo haki,
ulimwengu umekuwa uwanja wa mapambano
4.
Maisha yangu yamekuwa ya mashaka na ya hofu, wauaji wametanda kila kona,
wachinjao bila hofu kwa ajili ya dunia
5
.Ee Yesu wangu fanya hima uniokoe mimi, nakungoja uje uniokoe, nakusubiri
Mwokozi uje uniokoe.