Ingia / Jisajili

Umenifilia Mimi

Mtunzi: Martin Mutua Munywoki
> Tazama Nyimbo nyingine za Martin Mutua Munywoki

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Juma Kuu

Umepakiwa na: Martin Munywoki

Umepakuliwa mara 644 | Umetazamwa mara 2,212

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

1. Ulimwengu umekuhukumu, kwa ajili ya dhambi za wanadamu,

Umeteseka umemwaga damu, mkononi mwao watu wadhalimu
Umefanya lipi kosa, jinsi wanavyokutesa
Au lipi lilokupasa, kulitenda ukakosa,
Uteseke jinsi hii, mtini mtupu kabisa,
Umenifilia mimi, nipate uzima wa milele

2. Wafuasio wamekukimbia, ulo nao wanasinziasinzia,
Yule mtume uloaminia, mtunza fedha Yuda kakusalitia,
Uliyemkweza mwamba, ushujaa unayumba
Sasa Petro akana kwamba, hakujui pale chemba,
Na wewe husemi neno, ki-nywa chako umefumba
Umenifilia mimi, nipate uzima wa milele

3. Yule jambazi wamemweka huru, ila wewe mauti  wameamuru, 
Pilato ashindwa kukunusuru, mbele ya umati upigao nduru,
Unapewa msalaba, kichwani taji la miiba
Mijeledi unapobeba, na makofi wakuzaba
Mwili wote ni vidonda, unapumua haba haba
Umenifilia mimi, nipate uzima wa milele

4. Wakudhihaki wakuchekelea, hata mate wakutemea temea,
Lakini nawe unawaombea, husimami hata ukajitetea
Vazio wamekupora, wanalipigia kura,
Na yule mamao bikira, machozi yamfumba sura,
Mkuki wanakuchoma, wanyweshwa siki kukukera
Umenifilia mimi, nipate uzima wa milele

5. Ulipokuja humu duniani, ni mapendo katutoe utumwani
Umejitoa ufe pale mtini,  ili mwisho tufike juu Mbinguni
Ni pendo zaidi gani, kupita hili jamani,
Kuuweka uhai chini, kwa rafiki wa thamani
Asante kutukomboa milele milele milele
Umenifilia mimi, nipate uzima wa milele


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa