Ingia / Jisajili

Hazina Mbinguni

Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Basil Tumaini

Umepakuliwa mara 6,692 | Umetazamwa mara 13,267

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

HAZINA MBINGUNI

Mathayo 6:19-21

Mtunzi: Dr Basil B. Tumaini (0767847258)

 

Kiitikio

Jiwekeeni hazina yenu, hazina yenu mbinguni (mbinguni)

kusiko haribika kitu,

kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji;

Jiwekeeni hazina yenu mbinguni.

kwa nondo wala kutu, wala wevi hawaibi;

Jiwekeeni hazina yenu mbinguni.

 

Viimbizi

1. Msijiwekee hazina duniani

    nondo na kutu viharibupo

    na wevi huvunja na kuiba.

2. Bali jiwekeeni hazina yenu mbinguni

    kusikoharibika kitu

    kusikoharibika kitu.

3. Kwa kuwa hazina yako ilipo

    ndipo na moyo wako utakapokuwa

    ndipo na moyo wako utakapokuwa.

 

 


Maoni - Toa Maoni

Emanuel Omondi Mikoyo Jan 04, 2023
Wimbo tamu Sana. Napenda hii wimbo kwenye misa takatifu. Ubarikiwe sana

Toa Maoni yako hapa