Ingia / Jisajili

Bwana Yu Karibu

Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Basil Tumaini

Umepakuliwa mara 2,160 | Umetazamwa mara 4,835

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

BWANA YU KARIBU

Mtunzi: Dr. Basil Tumaini

Wimbo wa katikati: Jumapili ya 25 A.

Zaburi ya sifa kwa Bwana, Mfalme.

Kiitikio: (Zab. 145:18)

Bwana yu karibu, Bwana yu karibu na wote wamuitao, x 2

Nao wote wamwitao Bwana kwa uaminifu.

Na wote wamuitao Bwana kwa uaminifu. X 2

Mashairi (Zab. 145:2-3, 8-9, 17-18)

1.    Kila siku nitakuhimidi, nitalisifu jina lako milele na milele.

Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, wala ukuu wake hautambulikani.

2.    Bwana anafadhili, ni mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira ni mwingi wa rehema.

Bwana ni mwema kwa watu wote; na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.

3.    Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.

Bwana yu karibu nao wote wamwitao, wote wamwitao kwa uaminifu.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa