Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini
Makundi Nyimbo: Shukrani | Zaburi
Umepakiwa na: Basil Tumaini
Umepakuliwa mara 2,875 | Umetazamwa mara 6,925
Download Nota Download MidiNITAKUSHUKURU
Mtunzi: Dr. Basil Tumaini
Wimbo wa Shukurani na sifa (taz. Zab. 138)
Kiitikio:
Nitakushukuru Bwana kwa neema zako
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitakuimbia nyimbo za kukushukuru,
Kwa sauti tamu nitaimba sifa zako,
Kwa kinanda pia ngoma nayo matoazi,
Nitazitangaza sifa zako Mungu wangu.
Nitayatangaza matendo yako makuu,
Na fadhili zako nitaziimba milele.
Mashairi:
1. Siku ile niliyokuita uliniitikia, ukanifariji nafsi yangu kwa kunitia nguvu.
2. Wafalme wote wa dunia watakushukuru, watakapo yasikia maneno ya kinywa chako.
3. Ingawa Bwana yuko juu amuona mnyenyekevu, naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
4. Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, na mkono wako wa kuume utaniokoa.
5. Bwana atanitimilizia mambo yangu, maana fadhili zake Bwana ni za milele.