Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Basil Tumaini
Umepakuliwa mara 1,611 | Umetazamwa mara 5,295
Download Nota Download MidiKARIBU MAISHANI MWANGU
Mtunzi: Dr. Basil Tumaini
Wimbo wa sifa, shukrani na maombi kwa Bwana Mfalme.
Kiitikio:
Karibu maishani mwangu Ee Bwana Yesu:
Unifanye niwe chombo cha amani yako.
Karibu maishani mwangu Ee Bwana Yesu:
Unifanye niwe chombo cha upendo wako.
Tawala moyo wangu
Tawala nyumba yangu (Bwana)
Tawala vyote vyangu
Ee Bwana Mungu wangu x 2
Mashairi:
1. Asante kwa mema yako
Ni mengi siwezi taja
Maana u mwema sana
Ee Mungu wangu
Kwa nyimbo nitakusifu
Kwa nyimbo nitashukuru
Kwa nyimbo nitakuomba
Ee Mwenyezi mungu
2. Ongoza maneno yangu
Ongoza matendo yangu
Ili nikutumikie
Wewe siku zote
Niumbie moyo safi
Nitii sheria zako
Uovu unisafishe
Nikutumikie
3. Bariki wa nyumba yangu
Bariki wazazi wangu
Bariki na mali zangu
Ee Mwokozi wangu
Bariki taifa letu
Bariki kanisa lako
Tujaze amani yako
Ee Mungu wetu
4. Bariki shughuli zangu
Fanaka unijalie
Kwa hizo nikutukuze
Wewe siku zote
Nijaze imani kwako
Nijaze mapendo kwako
Nipe na hekima yako
Ee Mungu wangu